Linapokuja swala la kuchagua computer kwaajili ya kufanyia kazi za graphic & designing ni swala ambalo linahitaji bajeti nzuri ili kupata matokeo bora. Wengi wetu huwa tunafanya graphics lakini computer zetu hazijakizi vigezo vya kufanya hizo kazi.
Pale unapoamua kununua computer kwa ajiili ya graphic basi hakikisha usiwe mbahili wa kutoa fedha kwa sababu computer za aina hiyo huwa ni ghali sana ukilinganisha na computer za kawaida.
Hapa nimekuwekea vigezo vya chini kabisa (minimum requirements) ambavyo at least computer yako iwe navyo ili ifanye kazi za graphic.
1. Processor/CPU
Hakikisha unachagua computer yenye processor speed kubwa ili kufikia malengo kwa haraka. Angalau processor yako ianzie 1.9GHz ila kubwa zaidi ni bora kwani hiyo itakuwa inafanya kazi slow sana.
2. RAM
Hiki ni kipengele muhimu sana katika kufanya kazi kwa haraka zaidi. Nashauli angalau uwe na RAM kuanzia 8GB na kuendelea chini ya hapo sidhani kama unaweza kutoboa na ukifanikiwa basi pc yako itakuwa slow sana.
3. VRAM/GPU GRAPHICS CARD
VRAM ni Video Random Access Memory hii husaidia kupata quality ya kazi pia husaidia katika rendering za kazi. Sio program zote zinahitaji VRAM ila ni muhimu Pc iwe nayo angalau 2GB na kuendelea.
4. INTERNAL STORAGE (HDD/SSD)
Kwa matokeo bora na wepesi wa kuhifadhi kazi na kufanya running za program nashauli angalau uanzie 500 HDD/SSD na kuendelea.
5. NUMBER OF CORE (eg i3, i5, i7...)
Hii ni ile hali ya pc kufanya kazi nyingi kwa muda mchache (multitasking) bila ya kukwamakwama. Angalau uanzie Core i5 na kuendelea.
6. SCREEN RESOLUTION
Huu ni ulee ukubwa wa kioo cha computer yako ambapo angalau uanzie 1920x1080 pixels ili kupata picha angavu. Hili sio muhimu sana ila jambo la kuzingatia pia.
ZINGATIA, VIGEZO HIVYO NI KWAAJILI YA WALE WANAOTAKA KUTUMIA PROGRAM KUBWA KAMA PHOTOSHOP, ILLUSTRATOR N.K