r MAMBO 5 YA KUZINGATIA UKIWA KAMA DESIGNER

MAMBO 5 YA KUZINGATIA UKIWA KAMA DESIGNER


Ukiwa kama designer kuna mambo ya msingi unapaswa kuyafahamu ili uwe imara katika kutengeneza maudhui yako.

Wengi katika wale wanaoanza kujifunza huwa hawazingatii misingi ya designing hivyo hujikuta wanaishia njiani katika kazi zao.

Pia kutokuzingatia misingi hupelekea kufanya kazi zilizo chini ya ubora ukilinganisha na wengine.

HAYA NI MAMBO MATANO UNAYOPASWA KUYAZINGATIA :

1. PRINCIPAL OF DESIGN

Huu ndio msingi wa ubunifu ambao designer anapaswa kuzingatia. Msingi huu unahusisha matumizi sahihi ya rangi, mistari, nafasi na vitu vingine kabla ya kuanza kazi yako.

2. UCHAGUZI WA SOFTWARE & PROGRAM

Baadhi ya kuamua ni kitu gani unafanya, wapaswa kuchagua ni program gani utaenda kutumia katika kazi yako. Uchaguzi usio sahihi hupelekea matokeo tofauti na ulivyotarajia.

3. KUWA KARIBU NA WATU (WANAO FANYA KAZI KAMA ZAKO AU WAZOEFU KATIKA MASOKO)

Ili uweze kupata soko mapema, unatakiwa kuweka ushirikiano bora kati yako na watu walio juu yako ili panapotokea uhitaji wa mfanyakazi iwe rahisi kupatikana.

4. KUCHAGUA ENEO UTAKALO HUSIKA NALO

 Kwa upande huu, designer hupaswi kuhusika na maeneo mengi kwa wakati mmoja ukiwa unaanza. Unapaswa uchague ni sehemu ipi sahihi uwe una deal nayo.

Mfano, photo editing, video editing au photography.

5. KUCHAGUA PORTFOLIO

Ili uweze kutoa kazi bora ni vema uanze na kulinganisha kazi yako na wengine wamefanya nini. Pia kubali kujitolea pale inapohitajika ili kukuza uwezo wa kudisign vilevile huongeza nafasi ya kupata ajira.

 Nahisi umejifunza kitu, hivyo wewe kaamam designer fanya uchaguzi sahihi kabla ya kuanza kazi ya kuandaa maudhui.

Mpya zaidi Nzee zaidi